Kauli ya DIAMOND Platnumz Yamfanya Mrisho Mpoto Asitishe Kuachilia Video ya 'Sizonje'
Kauli ya staa wa muziki Diamond Platnumz ‘Kuna kushoot video na
kurekodiwa’ imemfanya msanii wa muziki wa asili Mrisho Mpoto kuitia
kapuni kwanza video yake mpya ya wimbo ‘Sizonje’ ili aichunguze kwanza
kama inafaa.
Kupitia ukurasa wa instagram, Mpoto ameandika;
"Diamondplatnumz post
yako ya leo imenifanya nisile Siku nzima. Nikiitafakari na sasa nimeamua
kusitisha kutoa video yangu mpya ya #SIZONJE maana sina uhakika kama
nime shoot au nimerecord. Ukimkimbiza sana mjusi anageuka kuwa nyoka"
Ijumaa hii Diamond aliachia video mpya ya wimbo ‘Make Me Sing’ akiwa na AKA wa Africa kusini na kutwitter.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Filed Under:
WASANII
on Sunday, February 14, 2016
Note: Only a member of this blog may post a comment.