Stori: Erick Evarist, Wikienda
DAR ES SALAAM: BAADA ya mvutano wa muda mrefu, hatimaye diva wa Bongo
Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ amepewa talaka rasmi kwenye Mahakama
ya Manzese, Sinza jijini Dar.
Jide alifungua kesi ya madai ya talaka katika mahakama hiyo baada ya
kutofautiana na mtangazaji maarufu Bongo, Gardner G. Habash ‘Captain’,
aliyekuwa mumewe wa ndoa kabla ya kumwagana takriban miaka miwili
iliyopita.
Gardner G. Habash ‘Captain’
Taarifa kutoka kwa chanzo cha kuaminika,
wawili hao waliooana mwaka 2005, walitinga katika viunga vya mahakama
hiyo Alhamisi iliyopita kisha hukumu ya kesi hiyo kusomwa na talaka
rasmi kutolewa kwa Jide na Gardner.
“Nimemuona Jide na Gardner hapa, wamekuja kusikiliza hukumu yao.
Taarifa za uhakika ni kwamba tayari mahakama imevunja rasmi ndoa na kila
mmoja kapewa hati yake ya talaka na sasa kila mtu yupo huru kuendelea
na maisha yake,” kilisema chanzo.
Baada ya taarifa hizo kutua kwenye dawati la gazeti hili, mwanahabari
wetu alimtafuta Jide ili aweze kuzungumzia hatua hiyo waliyoifikia
lakini simu yake haikuwa hewani kama ilivyokuwa kwa Gardner lakini
bahati nzuri mmoja wa ndugu wa mrembo huyo mkongwe wa Bongo Fleva
aliyeomba hifadhi ya jina alipatikana na kufunguka:
“Ni kweli tulikuwa mahakamani. Jide ameshapewa talaka yake na kila
kitu kimeenda vizuri. Gardner naye kapewa hati yake ya talaka hivyo
kuanzia sasa kila mmoja yupo huru kufanya yake.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.