Saturday, December 12, 2015

Anonymous

Sijaridhika Wala Kukubaliana na Utumbuaji wa Majipu wa Huyu Mheshimiwa MAGUFULI Kutokana na Haya


Sijaridhika wala kukubaliana na utumbuaji wa majipu wa huyu Mheshimiwa Magufuli, ambaye ni Rais wa Jamhuri yetu ya Muungano.
Jambo la kwanza alilonikosesha nisimwamini kwa asilimia kubwa niusanii namna alivyokwepesha kashfa ya watu binafsi waliojimilikisha UDA na kuikosesha serikali mapato kwa kukwepa kodi. Suala la UDA limefukiwafukiwa hadi sasa linaonekana kutopewa uzito stahiki.

Uteuzi wa baraza la mawaziri umedhihirisha hana jipya zaidi ya kuwanyanyapalia dagaa huku wahusika wakuu wa kashfa bandarini, Escrow na TRA waliokuwa mawaziri na makatibu wakuu wa serikali ya Kikwete akiwatunukia uwaziri tena na kuendelea Ukatibu Mkuu licha ya kashfa nzito zilizoibuliwa na bunge hadi kuachia ngazi.

Kushindwa kushughulikia mgogoro wa Uchaguzi Mkuu Zanzibar dalili tosha Rais Magufuli kadiri ya msimamo wa CCM hana ubavu kwa chama chake, bali kukipigia magoti tu. Hana nguvu alina nayo kikatiba ila kutii matakwa ya chama chake.
Dhahiri alichoanza Rais Magufuli ni nguvu za soda, hatimaye yatakayojilia ni kukata tamaa na kuendelea na mazoea bora liende muhula uishe.
Source: Jamii Forums

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.