
Katika taarifa hiyo Profesa Mchome amesema utamaduni huo wa kuongeza ada kila fikapo mwishoni mwa mwaka umekuwa ukisababisha usumbufu mkubwa kwa wazazi na walezi na hata baadhi yao kushindwa kuendelea kusomesha vijana wao katika baadhi ya shule.
Taarifa hiyo imesema kuwa ada zote kwa shule zisizo za serikali zitabaki kama zilivyo idhinishwa na kamishina wa elimu, wamiliki wa shule hizo wametakiwa kuwasilisha taarifa kwa msajili wa shule aliyeko idara ya ithibati ya shule inayo eleza kiasi cha ada kinachotozwa kwa sasa na tarehe shule kutoka kwa kamishina wa elimu.
Note: Only a member of this blog may post a comment.