Kasi ya utendaji kazi wa Rais wa awamo ya tano Dr. John Pombe Joseph
Magufuli inazidi kuwagusa wengi, sasa time hi imegusa msanii kutoka Tip
Top Connection, Madee ambaye anatamani kuona fedha watakazolipwa
mawaziri zitumike kujenga barabara za juu (Flyover) kutoka Ubungo mpaka
Manzese
Msanii huyo akiongea na ripota wa millardayo alisema..’Kitu
ambacho ninachokiona ni kwamba Mh Rais amesimamia Zaidi kwenye suala
zima la uchumi alichotaka yeye kurudisha Uchumi ambao tayari ulikuwa
umetetereka kwasababu unaona tunanunua vitu kwa gharama dola imepanda
alichokifaya cha kwanza amekata zile posho za wabunge’ ->>> Madee
‘Kingine ambacho nimekiona amepiga
marufuku vikao ambavyo vilikuwa vinafanyika katika mahoteli makubwa
kwani vilikuwa vinatumia gharama kubwa, pia amekataka maadhimisho ya
siku ya Ukimwi Duniani tutasheherekeaje wakati watu wanaumwa hii ni kitu
mbaya kwa hiyo Mh Rais Magufuli alichoamua hizo hela zinazotumika
katika maadhimisho basi zinatumika kununua Dawa’ ->>> Madee
‘Ndio maana nikatamani hela ambazo
wanalipwa mawaziri kwanini zisije kutengeneza barabara za juu yaani
Flyover kutoka Ubungo ipite Manzese na Posta nadhani ingekuwa suala zuri
sana hiyo mishahara ya mawaziri’ ->>> Madee
Note: Only a member of this blog may post a comment.