Hatimaye majina ya wanaowania tuzo za Kora 2016 yametangazwa rasmi leo Dec.3 , ambapo Tanzania inawakilishwa na wasanii watano.
Diamond Platnumz ametajwa kuwania kipengele cha Best Male- East Africa, huku Vanessa Mdee akiwania Best Female-East Africa. Wakazi anawania kipengele cha Best Hip Hop, na Yamoto Band wametajwa kuwania kipengele cha Most Promising Male Artist Of Africa, bila kumsahau Mrisho Mpoto anayewania Best Traditional Male Artist Of Africa.
Mbali na tuzo yenyewe zawadi kubwa ya mwaka huu kwenye kipengele cha ‘Best Artist of the Continent’ itakuwa ni 1,000,000$ USD sawa na zaidi ya shilingi bilioni 2.
Washindi wa vipengele vya Best Male Artist – West Africa, Best
Female Artist -West Africa , Best Male Artist -East Africa, Best Female
Artist – East Africa, Best Male Artist – Central Africa, Best Female
Artist – Central Africa, Best Male Artist of Southern Africa, Best
Female Artist – Southern Africa ,Best Male Artist -North Africa na Best
Female Artist -North Africa watapata 50 000$ USD sawa na zaidi ya shilingi milioni 100 kila mmoja.
Washindi wa vipengele vyote vilivyosalia watapata zawadi ya 20 000$ USD sawa zaidi ya shilingi milioni 43 kila mmoja.
Hapo mwanzo tuzo za Kora zilipangwa kufanyika December 13, 2015 Namibia, na mwisho wa kupokea maombi ya wasanii waliotaka kushiriki ilikuwa ni July 20, 2015.
Tuzo hizo sasa zitatolewa March 20, 2016 huko Windhoek, Namibia.
Hii ni orodha kamili ya wanaowania Tuzo za Kora 2016
<img src="http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2015/12/kora4.jpg" alt="kora4" width="600
Note: Only a member of this blog may post a comment.