Friday, December 4, 2015

Anonymous

Uwaziri wa MAGUFULI wa Moto, Wabunge Wengi Waugwaya!

Kuna sababu za kwanini hadi sasa Rais Dk John Magufuli hajatangaza baraza lake la mawaziri licha ya kuwepo ofisini kwa takriban mwezi sasa.

Taarifa zinadai kuwa uwaziri kwenye serikali yake ni mwendo ‘msobe msobe’ na si ule wa kula bata na safari kibao za nje kama ilivyokuwa awamu iliyopita, ndio maana wabunge wengi wanaugwaya.
Infact ndugu yako akiteuliwa na Magufuli kuwa waziri mpe pole badala ya kumpongeza kuwa ameula! Ule usemi Hapa Kazi tu si wa mdomoni na kuvutia kura tu, ndani ya siku chache alizozitumia tangu aapishwe kuwa rais, Magufuli amefanya mambo makubwa ambayo kwa rais wa ‘business as usual’ angetumia mwaka mzima.

Uwaziri wa Magufuli una masharti magumu. Ukizingua kwa kuruhusu ufisadi, ama zako ama zake na huenda ukaishia kupoteza heshima yako na kifungo juu.
Magufuli anataka mawaziri watakaouweza muziki wake na ndio maana inadaiwa kuwa anaanda mikataba maalum yenye maelezo marefu ya kusoma siku mbili! Huenda ukimaliza kuusoma mkataba huo ukahitaji ugali mkubwa wa kupoza njaa kutokana na uzito wake.

Taarifa zinadai kuwa Magufuli anatumia muda kuchambua majina ya wabunge majembe watakaopiga kazi na pia kufikiria kuchukua hata watu walio nje ya mfumo wa bunge.
Anataka mawaziri ambao watatambua kuwa wameteuliwa kupiga mzigo kwaajili ya wananchi na sio kujitajirisha kwa madeal ndani ya wizara zao.

Mitaa inatonya kuwa wabunge waliokuwa bega kwa bega na Magu kwenye kampeni wakitarajia kupewa mashavu ya uwaziri, wamegundua mwana si wao tena na kwa mkwara wake wa tangu ashike hatamu, hawana tena hamu.
“Heri nusu shari kuliko shari kamili.”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.