Jina la Nasib Abdul bado halijatoka kichwani mwa Wema Sepetu!
Nasib Abdul ni jina halisi la Diamond Platnumz.
Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 na muigizaji wa filamu alikuwa
akijibu swali kwenye kipindi cha Hitzone kupitia kituo cha redio cha
Jembe FM cha jijini Mwanza alipoulizwa ni mwanaume gani ambaye alitamani
awe mume wake wa ndoa.
“Ni yupi ambaye niliwahi kusema huyu anaweza kuwa wa maisha,” alisema
Wema. “Kiukweli alikuwa anaitwa Nasib Abdul,nilishawahi kusema hivyo,”
alisisitiza.
Hata hivyo ndoto hiyo iliyeyuka baada ya wawili hao kuachana mwaka
jana na Diamond kuhamisha mahaba yake kwa Zari the Bosslady ambaye
tayari wana mtoto wa kike, Tiffah.
Note: Only a member of this blog may post a comment.