Tuesday, November 3, 2015

Anonymous

Sehemu ya Pili Hekaheka ya Watu Kuchomwa Moto na Waendesha Bodaboda Buguruni.. (+Audio)

Hii stori ni ya kuhuzunisha, tukio lilianza kusimuliwa jana kwenye Hekaheka ambapo watu wawili walipigwa na waendesha bodaboda wakituhumiwa kwa wizi wa pikipiki eneo la Buguruni Dar.
Dada mmoja ambaye amesurika kuuawa kwenye tukio hilohilo amesimulia juu ya ishu yote ilivyokuwa… mpenzi wake alikamatwa na kupelekwa eneo la Sukita Buguruni, wakampiga na kumchoma moto… mwanamke huyo alipigiwa simu kwamba mpenzi wake anauawa !!

Baada ya dada huyo nae kwenda eneo hilo, na yeye walimkamata na kumpiga huku wakitaka kumchoma moto kama ambavyo mpenzi wake amefanywa, kisa cha hayo ni kwamba walimtuhumu pia dada huyo kushirikiana na mpenzi wake kwenye wizi.

Baadae Polisi walimwokoa dada huyo na kwa sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Muhimbili… ukisikiliza sauti ya Hekaheka hapa utamsikia na dada mwenyewe akiwa kwenye matibabu Muhimbili.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.