Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.
DAR ES SALAAM
ASKARI Polisi
wa Kituo cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Wachuku Lotson Mwaipasi (51)
ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi, wakati
akijaribu kumsaidia binti yake aliyekuwa akitaka kuporwa dukani huko
Bunju, nje kidogo ya jiji wiki iliyopita.
Inadaiwa kuwa hiyo ni mara ya pili kwa
askari huyo kuvamiwa dukani kwake ndani ya muda mfupi, kwani Agosti
mwaka huu, watu wanaodhaniwa kuwa wezi walifika na kutaka kupora.
Inadaiwa kuwa kabla ya mauaji hayo
kutekelezwa na wenyewe kutokomea kusikojulikana, majambazi hao walivamia
maduka mengine na kupora fedha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP
Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema msako
mkali unaendelea kuhakikisha wauaji hao wanatiwa mbaroni.
Alisema idara ya upelelezi itafanya kazi
yake kwa haraka ili kuwanasa watu hao huku akitaka kupewa maendeleo ya
msako huo kila mara.
Marehemu Mwaipasi alizikwa nyumbani kwao mkoani Mbeya Novemba 4, mwaka huu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.