Maximillian Katikiro, enzi za uhai wake .
Na Makongoro Oging’na Haruni Sanchawa
DUNIA mbaya! Ni
tukio lililowashangaza wafanyakazi wa hospitali kubwa ya binafsi
nchini, Regency iliyopo jijini Dar pale walipopata taarifa za kuuawa kwa
Mkuu wa Kitengo cha Information Technology (IT), Maximillian Katikiro
(35) usiku wa kuamkia Novemba 2, mwaka huu.
Shughuli za maziko kwa marehemu.
Uwazi baada ya kupata
taarifa za msomi huyo kuuawa lilifika nyumbani kwa wazazi wake, Gongo la
Mboto, Dar na kukutana na baba mzazi wa marehemu.
Katika mahojiono kuhusiana na kifo cha
mwanaye, mzee Katikiro alisema siku ya tukio, kijana huyo akiwa kwake
Kitunda alimuaga mkewe anakwenda Yombo kukutana na mtu kwa mazungumzo ya
biashara.
Alisema marehemu alichelewa kurudi hivyo ilifika wakati mkewe akaanza kumtafuta kwenye simu lakini akawa hapatikani.
Usiku sana, mke wa marehemu alitoa
taarifa kwa wakwe zake, pia alimpigia simu rafiki yake mmoja na
kumtaarifu kuwa, mume wake hajarudi na simu yake haipatikani kitu
ambacho si kawaida yake.
“Yule rafiki wa mke wa Maximillian
alikwenda nyumbani kwa marehemu Kitunda, wakaungana na kuanza kutafuta
vituo vyote vya polisi na meneo mengine. Kilichosikitisha ni kwamba,
walifika sehemu wakakuta mwili wa Maximilian umetupwa maeneo ya
Mwanagati, hatua kadhaa kutoka nyumbani kwa marehemu.
Akaendelea: “Nilihakikishiwa kuwa ni
mwanangu, wakaniuliza wanafanyaje jibu nililowapa ni kuwa msiba uletwe
hapa nyumbani Gongo la Mboto kwa maana ya kuanza taratibu nyingine
pamoja na uchunguzi kisha maziko.”
Hata hivyo, taarifa zilizonaswa na
gazeti hili zinaonesha kuwa, siku ya tukio marehemu alikodi bodaboda
sehemu kwenda nyumbani kwake, Kitunda kwa mapatano ya malipo ya shilingi
2,500.
Inadaiwa kuwa, walipokaribia marehemu
alimwambia dereva amefika akamlipa shilingi 2,000 hivyo marehemu
alipungukiwa shilingi mia tano jambo ambalo bodaboda hakukubaliana
nalo.
Taarifa hizo zinasema kuwa kwa kupishana
lugha, marehemu alimwambia dereva amrudishe alikomtoa jambo ambalo
dereva alikubaliana nalo.
“Alipomfikisha kule, dereva aliwaambia wenzake kuwa, abiria huyo amemzingua, hataki kumlipa pesa yake.
“Nasikia wenzake walianza kumshambulia
marehemu mpaka kumuua kisha kwenda kuutupa mwili eneo la Mwanagati,”
kilisema chanzo kimoja.
Marehemu Maximillian alizikwa wiki iliyopita katika Makaburi ya Air Wing, Ilala jijini Dar es Salaam.

Note: Only a member of this blog may post a comment.