Monday, November 9, 2015

Anonymous

PICHAZ: TAIFA STARS YAFANYA MAZOEZI YA MWISHO SAUZ

Taifa Stars (1)
Wachezaji wa Stars wakisikiliza maelekezo kutoka kwa kocha wao, Charles Boniface Mkwasa.
Taifa Stars (2) Taifa Stars (3)
Stars wakiendelea kujifua nchini Afrika Kusini leo.
Taifa Stars (4) Taifa Stars (5)
Mkwasa akitoa maelezo kwa vijana wake.
Taifa Stars (6)Mazoezi ya mwisho yakiwa yamepamba moto.
KIKOSI cha timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars leo kimefanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Edenvale jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Kikosi hicho kilichoweka kambi nchini humo kwa ajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria, kesho kitakwaana na timu ya U-23 ya Afrika Kusini na Jumatano kitarejea nyumbani tayari kwa mpambano wake na Algeria.
Stars watakipiga na Algeria katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018 Jumamosi ya Novemba 14, mwaka huu jijini Dar er Salaam kabla ya kurudiana Novemba 17 jijini Algiers.
(PICHA ZOTE NA SALEH ALLY / GPL, AFRIKA KUSINI)

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.