Monday, November 9, 2015

Anonymous

CHAMA KIPYA CHA SIASA CHAZINDULIWA DAR

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi (kushoto) akimkabidhi cheti cha usajili wa mmoja wa waanzilishi wa chama hicho, Deonatus F. Mutani kwenye Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa jijini Dar.
Waanzilishi wa chama kipya cha Tanzanian Patriotic Front, Deonatus F. Mutani (aliyeshika cheti) na Optatus B. Likwelile wakionesha cheti kwa wanahabari.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza (kulia) akizungumza jambo. Kulia kwake ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.
Wanahabari wakichukua matukio.
CHAMA kipya cha siasa nchini kijulikanacho kama Tanzanian Patriotic Front, kimezinduliwa jijini Dar na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Fransis Mutungi kutoka kwa waanzilishi wa chama hicho, Deonatus F. Mutani na Optatus B. Likwelile. 

Chama hicho kimezinduliwa leo kwenye Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa jijini Dar mbele ya waandishi wa habari ambao walishuhudia waanzilishi wa chama hicho wakipewa cheti cha usajili. 

Katika uzinduzi huo, Jaji Mutungi amesema kwa mujibu wa sheria na taratibu za usajili wa vyama, waanzilishi wa chama hicho watakiwa kuhakikisha wanafuata vigezo vinavyohitajika ikiwemo kuzunguka mikoa 10 ya Tanzania Bara na Serikali ya Zanzibar kupata wanachama wasiopungua 2000 ili kuweza kupata usajili wa kudumu. 
(NA DENIS MTIMA/GPL)

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.