Akiwa haamini anachokiona.
Deogratius Mongela na Chande Abdallah
MSHTUKO! Mama mmoja mke wa kigogo mfanyabiashara, aliyetajwa kwa jina moja la Catherine, mkazi wa Mbezi Beach Libermann jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alipagawa vibaya wakati jumba lake la thamani likivunjwa na wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni waliokuwa wakipewa ulinzi mkali na polisi.
MSHTUKO! Mama mmoja mke wa kigogo mfanyabiashara, aliyetajwa kwa jina moja la Catherine, mkazi wa Mbezi Beach Libermann jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alipagawa vibaya wakati jumba lake la thamani likivunjwa na wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni waliokuwa wakipewa ulinzi mkali na polisi.
Mwanamke huyo, alijikuta kwenye wakati
mgumu baada ya nyumba yake inayodaiwa kuwa na thamani ya shilingi
Milioni 500 kuvunjwa kwenye zoezi la bomoabomoa linaloendelea jijini Dar
es Salaam.
Katika eneo la tukio, gazeti hili
lilimshuhudia mke huyo akionekana kuchanganyikiwa, akiwasihi maofisa wa
halmashauri hiyo kuacha kutekeleza kusudio lao, kwani suala la nyumba
hiyo lilikuwa mahakamani, jambo ambalo lilipingwa na zoezi hilo
kuendelea bila pingamizi.
Akikwepa kupigwa picha.
Akiwa haamini kilichoendelea, mama huyo
alichukua dumu la maji lenye ujazo wa lita tano na kuanza kuzunguka nalo
huku na huko, akinywa maji na kuzungumza kwa simu na ndugu zake wa
karibu, kiasi cha kuwashangaza mashuhuda, waliojiuliza kwa nini
hakuchukua chupa ndogo ya lita moja!
Inadaiwa kuwa mume wa mama huyo
aliyetajwa kwa jina moja la Deusdedith, alivamia kiwanja hicho Block J
712 zaidi ya miaka 10 iliyopita na baada ya mmiliki wake halali, Protax
Bilali kwenda mahakamani, alishinda kesi lakini mvamizi huyo alikaidi
amri ya kuondoka eneo hilo hadi sheria ilipochukua mkondo wake wiki
iliyopita.
“Mama amesema mumewe amempigia (jina
linahifadhiwa, la mtoto wa rais mstaafu) lakini akamwambia yeye hawezi
kumsaidia, labda ampigie kigogo wa ardhi ambaye pia amemwambia zoezi
hilo ni gumu kwa sasa, mama amepagawa kabisa,” alisema shuhuda mmoja
mbele ya gazeti hili.
Katika kipindi cha siku tatu,
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imevunja jumla ya nyumba 26
zilizojengwa katika maeneo ya wazi na yaliyovamiwa na kwa mujibu wa
Injinia Baraka Mkuya wa manispaa hiyo, zoezi hilo litaendelea baada ya
wiki mbili.

Note: Only a member of this blog may post a comment.