CHA KUFIA! Msanii wa muziki wa Injili Bongo, Emmanuel Mbasha, Alhamisi iliyopita alinaswa kwenye maongezi yaliyoambatana na pozi lenye maswali kwa kuonekana akichukua namba fastafasta kwa mrembo ‘kifaa’.
Katika tukio hilo, wawili hao walikuwa kwenye kona wakitafuna vipapatio vya kuku na kubadilishana mawazo huku kila mmoja akimuonesha mwenzake tabasamu la amani na upendo.‘Wapiga chabo’ waliowaona walifika mbali zaidi kwa kusema eti, Mbasha akiishi na kifaa hicho watapendezana kwani anafanana na mkewe waliyetengana, Flora.
Akizungumza na Amani kuhusu mdada huyo, Mbasha alisema ni shabiki wa kazi zake na hana mpango wa kuziba nafasi ya Flora.

Note: Only a member of this blog may post a comment.