Thursday, November 12, 2015

Anonymous

MRISHO MPOTO AOMBWA KUGOMBEA UBUNGE, AMTOSA MANJI!

MPENZI msomaji wa simulizi hii tamu ya Mrisho Mpoto, wiki iliyopita tuliishia pale alipoanika baadhi ya mali zake na pia akaelezea kwa kina kuhusiana na shamba alilolitenga la ekari 35 kwa ajili ya kusaidia vijana kimuziki.
Songa nayo sasa...
Kwa nini Mrisho huwa hupendi kumwanika mkeo?
(anacheka, anatikisa kichwa...)
“Kikubwa ni kwamba mke wangu ni mtu ambaye tunafahamiana sana tangu kitambo (sijawa na jina) alikuwa na mapenzi ya kweli kabisa kwangu mpaka nimekuwa maarufu.“Amezaliwa kwenye mfumo wa dini ya Kiislamu (swala tano) tangu nakua alikuwa ameona jina langu lilivyokuwa linakua na alishawahi kuniambia ninachokifanya ni sehemu ya kazi hivyo hawezi kuniingilia.

“Naweza kusema kuwa, mke wangu amekuwa mshauri mzuri katika kazi zangu. Huwa hanichukulii kama mume wake tu bali kama shabiki wake namba moja. Hata ninapofanya mahojiano sehemu, yeye ndiyo husema mahojiano haya hayakuwa mazuri ama mabaya. Wakati mwingine nikiwa studio narekodi huwa hafichi, ananiweka wazi kuwa wimbo wako mbaya na kwamba mashabiki hawataupenda kama ukitoka.

Hata kwenye mavazi huwa hivyohivyo, huniambia kuwa nilivyovaa nimependeza ama sijapendeza, ulipokaa kwenye kile kiti wakati unahojiwa hukupendeza ama ulipendeza. Nadhani nimeeleweka kuwa mke wangu ni mtu wa aina gani kutokana na kutokaa kama mke wangu bali shabiki namba moja.”
Kumbee! Okey Mrisho tuachane na hilo, vipi kuhusu watoto wako, sijawahi kuwasikia sehemu yoyote na wao wamefuata nyendo za mama yao kuwa mashabiki tu?“Katika maisha yangu huwa sipendi kabisa kuwaanika watoto wangu kwa sababu nitawajengea usupastaa kutokana na mimi baba yao na kujikuta wakishindwa kutimiza malengo yao.

“Sipo tayari wafuate mfumo ambao wao wanautaka. Naamini mfumo bora wataupata kutokana na makuzi wanayokua nayo. Ninaweza kuwafanya wakawa wasanii wakubwa kumbe wao ndoto zao ni mainjinia, wengine madaktari. Hadi sasa nimewatengeneza tayari wanamchukulia baba yao ni mtu wa kawaida.

Ndiyo maana wakati mwingine wananiita Mjomba na siyo baba. Wakati mwingine nikiwa nao huniweka wazi kuwa baba nyimbo za mtu fulani ni nzuri kuliko zako. “Mfano mimi, nina watoto wa mtaani kibao ambao nawasomesha na wakati mwingine huwa nawapeleka watoto wangu katika vituo vyao wanaishi nao hata siku mbili au tatu na lengo kuu ni kuwajenga kisaikolojia kujua kuna watoto ambao wamepitia tabu. Kwa hiyo huwezi kukuta mwanangu nampa kipaumbele kwenye mitandano ya kijamii.”

Umeeleweka vizuri Mrisho, lakini kuna kitu kinanitatiza, vipi kuhusiana na harakati za siasa, hujawahi kufikiria kujitosa huko?

“Wanasiasa wengi nchini wameniomba kuingia kwenye siasa. Wananiambia ninaweza kufanya hiyo kitu na nina kila sifa inayotakiwa katika siasa za nchini.“Wanatambua kuwa nafasi ambayo nipo naweza kupeleka sauti kwa watu ambao hawana sauti (wanyonge) kwa sababu nimekuwa nikiwatetea sana.

“Najua wazi mpaka unakuwa mbunge unatakiwa kuripoti kwa mtu fulani zaidi lakini unapokuwa msanii huendi kuripoti kwa mtu mwingine. Kingine naogopa mashabiki wangu kugawanyika. Ninapochagua kugombea inamaana nakuwa upande mmoja wa chama hivyo kuna nafasi kubwa sana ya kuwachukuzia mashabiki wako walioko upande mwingine wagawanyike.

“Sipo tayari kujiingiza kwenye siasa hata nikipewa mabilioni ya pesa. Kipindi hiki kilichopita cha uchaguzi mkuu, wananchi wengi walikuwa tayari kunichangia nigombee ubunge, Mbagala. Mfano mmoja wapo ni Diwani wa Mbagala, Manji (Yusuf) aliniomba nigombee, nikamwambia siwezi kuingia kwenye siasa. Nitasapoti kwenye huduma za kimaendeleo tu.”
Simulizi hii bado inaendelea, unataka kujua zaidi kuhusiana na Mpoto? Tukutane wiki ijayo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.