ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Mpenzi msomaji wangu wiki iliyopita nilieleza namna ambavyo Wamarekani waliamua kusitisha safari za kwenda mwezini kwa sababu ya tishio la viumbe wa ajabu wanaodaiwa kuweka kambi mwezini.
Kuhusu viumbe hao wa Aliens na UFO, tayari watu zaidi ya nusu bilioni duniani kote wamefuatilia na wanaendelea kufuatilia habari hizo ambazo zimekuwa na msisimko mkubwa kwenye Vyombo vya Habari vya Magharibi.
SASA ENDELEA HAPA…
Nchi kubwa kama Urusi, Marekani, China, Uingereza na Japan, kwa muda mrefu sasa, zimekuwa na hofu kubwa juu ya Aliens. Kwamba viumbe hao wakipata nafasi ya kujitanua kiteknolojia hapa duniani itakuwa ndiyo mwisho wa ustaarabu wa binadamu. Inaelezwa kwamba ndiyo maana nchi hizo zinajitahidi sana kuzuia au kujipa wenyewe teknolojia yao ili itakapotokea Aliens wakavamia duniani, wao wawe tayari wamejiweka vizuri.
Wakati hali ikiwa hivyo, Machi 8, mwaka jana dunia ilisikia vilio vingi kutoka Beijing, China na Kuala Lumpur, Malaysia. Watu walikusanyika kwenye viwanja vya ndege wakiwalilia ndugu zao waliopotea kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia, Malaysia Airlines iliyokuwa imetoweka katika mazingira ya kutatanisha huku Aliens wakihusishwa.
Ndege hiyo ambayo ilikuwa ikifanya safari namba Flight 370 kutoka Malaysia kwenda China, ilipotea eneo la juu ya bahari katika Ghuba ya Thailand. Ukiondoa wafanyakazi na marubani, ilikuwa na abiria wapatao 239.
Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilitafutwa kila mahali lakini haikuonekana hadi baadaye iliporipotiwa kuonekana kwa bawa lake moja huko Kusini mwa Bahari ya Hindi.
Mataifa ya Marekani na China waliumiza vichwa kuitafuta ndege hiyo bila mafanikio.
Hata hivyo, ilielezwa kwamba tukio hilo halikuwa la mara ya kwanza kwani mwaka 2009, ndege kama hiyo ya Shirika la Ndege la Ufarasa nayo ilipotea duniani ambapo ilitafutwa bila mafaniko hadi miaka miwili baadaye mabaki yake yalipopatikana kwenye tope zito Kusini mwa Bahari ya Atlantiki.
Katika tukio la ndege ya Malaysia, baadhi ya wataalam wa mambo ya usalama wa vyombo vya anga, walizunguka angani na baharini ili kujua mahali ilipokuwa ndege hiyo.Kupotea kwa ndege hiyo kulitishia uhusiano wa China na Malaysia kwa tuhuma kwamba ulikuwa mpango.
Taarifa za awali zilisema kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na duniani saa chache baada ya kuruka. Baadhi ya watu walihoji kwamba kama ndege hiyo ilitekwa, ilipelekwa wapi hapa duniani?
Ilisemekana kwamba kama haikutekwa, basi ilitua mahali lakini kwa namna ambavyo teknolojia imekua ingejulikana tu.
Katika tukio hilo kulikuwa na maelezo kwamba ndege zote aina ya Boeing 777 huwa zina kisanduku maalum cha kutunzia kumbukumbu za mawasiliano ya marubani na waongoza ndege walioko ardhini kiitwacho Black Box. Hata kama ndege ikilipuliwa au kupata ajali ya nchi kavu au majini, hakiwezi kuharibika.
Kifaa hicho kina uwezo wa kurusha mawimbi kuonesha kilipo kwa siku zisizopungua 30 baada ya ndege kuanguka.
Lakini katika tukio hilo, wataalam walishindwa kunasa mawimbi ya chombo hicho na hivyo kuwa na wasiwasi kwamba huenda kiliharibiwa kwa makusudi.
Walidai kwamba hata kama ndege hiyo ilianguka baharini, kwa nini mabaki yake hayakuelea juu ya maji?
Kuna waliosema inawezekana ilipigwa kombora. Kama ndivyo, mbona kombora hilo halikuonekana kwenye vyombo vya uchunguzi vya kijeshi na vya usalama wa safari za anga? Ingepigwa kombora vingeonekana vipande vilivyosagika.
Wengine walidai kuwa ndege hiyo ilipoteza uelekeo na kuruka umbali mrefu wa saa saba kama ilivyoelezwa kisha kutoka nje ya nguvu ya mvutano (gravitational force) hivyo kushindwa kurudi duniani.
Je, nini kitaendelea? Usikose wiki ijayo.
Mpenzi msomaji wangu wiki iliyopita nilieleza namna ambavyo Wamarekani waliamua kusitisha safari za kwenda mwezini kwa sababu ya tishio la viumbe wa ajabu wanaodaiwa kuweka kambi mwezini.
Kuhusu viumbe hao wa Aliens na UFO, tayari watu zaidi ya nusu bilioni duniani kote wamefuatilia na wanaendelea kufuatilia habari hizo ambazo zimekuwa na msisimko mkubwa kwenye Vyombo vya Habari vya Magharibi.
SASA ENDELEA HAPA…
Wakati hali ikiwa hivyo, Machi 8, mwaka jana dunia ilisikia vilio vingi kutoka Beijing, China na Kuala Lumpur, Malaysia. Watu walikusanyika kwenye viwanja vya ndege wakiwalilia ndugu zao waliopotea kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia, Malaysia Airlines iliyokuwa imetoweka katika mazingira ya kutatanisha huku Aliens wakihusishwa.
Ndege hiyo ambayo ilikuwa ikifanya safari namba Flight 370 kutoka Malaysia kwenda China, ilipotea eneo la juu ya bahari katika Ghuba ya Thailand. Ukiondoa wafanyakazi na marubani, ilikuwa na abiria wapatao 239.
Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilitafutwa kila mahali lakini haikuonekana hadi baadaye iliporipotiwa kuonekana kwa bawa lake moja huko Kusini mwa Bahari ya Hindi.
Mataifa ya Marekani na China waliumiza vichwa kuitafuta ndege hiyo bila mafanikio.
Hata hivyo, ilielezwa kwamba tukio hilo halikuwa la mara ya kwanza kwani mwaka 2009, ndege kama hiyo ya Shirika la Ndege la Ufarasa nayo ilipotea duniani ambapo ilitafutwa bila mafaniko hadi miaka miwili baadaye mabaki yake yalipopatikana kwenye tope zito Kusini mwa Bahari ya Atlantiki.
Katika tukio la ndege ya Malaysia, baadhi ya wataalam wa mambo ya usalama wa vyombo vya anga, walizunguka angani na baharini ili kujua mahali ilipokuwa ndege hiyo.Kupotea kwa ndege hiyo kulitishia uhusiano wa China na Malaysia kwa tuhuma kwamba ulikuwa mpango.
Taarifa za awali zilisema kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na duniani saa chache baada ya kuruka. Baadhi ya watu walihoji kwamba kama ndege hiyo ilitekwa, ilipelekwa wapi hapa duniani?
Ilisemekana kwamba kama haikutekwa, basi ilitua mahali lakini kwa namna ambavyo teknolojia imekua ingejulikana tu.
Katika tukio hilo kulikuwa na maelezo kwamba ndege zote aina ya Boeing 777 huwa zina kisanduku maalum cha kutunzia kumbukumbu za mawasiliano ya marubani na waongoza ndege walioko ardhini kiitwacho Black Box. Hata kama ndege ikilipuliwa au kupata ajali ya nchi kavu au majini, hakiwezi kuharibika.
Kifaa hicho kina uwezo wa kurusha mawimbi kuonesha kilipo kwa siku zisizopungua 30 baada ya ndege kuanguka.
Lakini katika tukio hilo, wataalam walishindwa kunasa mawimbi ya chombo hicho na hivyo kuwa na wasiwasi kwamba huenda kiliharibiwa kwa makusudi.
Walidai kwamba hata kama ndege hiyo ilianguka baharini, kwa nini mabaki yake hayakuelea juu ya maji?
Kuna waliosema inawezekana ilipigwa kombora. Kama ndivyo, mbona kombora hilo halikuonekana kwenye vyombo vya uchunguzi vya kijeshi na vya usalama wa safari za anga? Ingepigwa kombora vingeonekana vipande vilivyosagika.
Wengine walidai kuwa ndege hiyo ilipoteza uelekeo na kuruka umbali mrefu wa saa saba kama ilivyoelezwa kisha kutoka nje ya nguvu ya mvutano (gravitational force) hivyo kushindwa kurudi duniani.
Je, nini kitaendelea? Usikose wiki ijayo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.