Mahakama Kuu nchini Mexico.
Mwanaharakati anayeunga mkono
matumizi ya bangi nchini Mexico, Lucha Libre aliyevaa Maski,
akishangilia mara baada ya Mahakama Kuu nchini humo kuruhusu matumizi ya
bangi.
Mmoja wa wavuta bangi raia wa Mexico akivuta msokoto wa bangi nje ya jengo la Mahakama Kuu ya nchi hiyo jana.
Mmea wa zao la bangi.

Watumiaji wa bangi nchini Mexico.
Mahakama Kuu nchini Mexico imehalalisha
zao la bangi litumike kwa kundia la watu wane tu ambao ni wanaharakati
nchini humo. Watu hao wane wameruhusiwa kupanda na kusambaza bangi kwa
matumizi yao wenyewe.
Hata hivyo sheria hiyo imetoa rukhsa kwa
watu hao wane pekee ambao ndiyo walikwenda mahakamani hapo kuomba
waruhusiwe kupanda na kutumia bangi.
Wachambuzi wa mambo wanadai kuwa sheria hiyo huenda ikafungua milango itakayoruhusu na kuhalalishwa matumizi ya bangi kwa jamii yote nchini humo siku zijazo.
Wachambuzi wa mambo wanadai kuwa sheria hiyo huenda ikafungua milango itakayoruhusu na kuhalalishwa matumizi ya bangi kwa jamii yote nchini humo siku zijazo.
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto
amesema kuwa sharia hiyo hiyo inazua mjadala kuhusu njia za kudhibiti
matumizi ma usambazaji wa madawa ya kulevya.
Wanaharakati wanasema kuwa kushindwa kwa
Mexico kuhalalisha matumizi ya bangi ndiko kulikowawezesha walanguzi wa
mihadarati kukolea katika biashara hiyo na kujivunia mabilioni ya
fedha.

Note: Only a member of this blog may post a comment.