Tausi Hamdani akiwa na watoto wake mapacha walioungana.
Na Haruni Sanchawa
Hujafa hujaumbika! Mtoto mwenye umri wa miaka 17, Tausi Hamdani (pichani), mkazi wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera amejifungua mapacha wa kike walioungana hivyo kujikuta kwenye wakati mgumu katika maisha yake.
Hujafa hujaumbika! Mtoto mwenye umri wa miaka 17, Tausi Hamdani (pichani), mkazi wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera amejifungua mapacha wa kike walioungana hivyo kujikuta kwenye wakati mgumu katika maisha yake.
Tukio hilo la kuhuzunisha limetokea
kijijini kwao, Rulenge kabla ya kufikishwa kwenye Hospitali ya Kata ya
Rulenge, Ngara mkoani Kagera.
Habari zilizolifikia Uwazi kutoka
kijijini hapo na kuzifanyia uchunguzi, zilieleza kwamba Tausi aliolewa
mwaka jana akiwa na umri wa miaka 16 na kijana aliyetajwa kwa jina la
Hamdani Tiholo mwenye umri wa miaka 20.
Diwani huyo alisema kuwa baada ya
kutokea tukio hilo, mama huyo alifikishwa kwenye Hospitali ya Rulenge
ili kusaidiwa kimatibabu katika kuwahudumia watoto hao waliohitaji
uangalizi maalum.
Mbali na diwani huyo, afisa mmoja wa
Wilaya ya Ngara ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kuwa mzazi
huyo alijifungulia katika Zahanati ya Nyaruma.
Afisa huyo alisema kuwa wazazi wote wa
watoto hao walioungana ni vijana wadogo wanaoishi katika mazingira ya
shida kwani hawana kazi ya kuwaingizia fedha.

Watoto mapacha walio ungana.
“Ilibidi ufanyike utaratibu wa
kumhamisha Tausi na watoto kwenda Hospitali ya Rulenge ambapo watoto
walikuwa wakinyonya maziwa ya mama yao lakini hatua zaidi zilikuwa
zinahitajika kwa ajili ya kuwapeleka katika Hospitali ya Rufaa ya
Bugando (Mwanza),” alisema afisa huyo.
Kwa mujibu wa taarifa za kiafya za
watoto hao, baada ya kuzaliwa Novemba 17, mwaka huu, watoto hao walikuwa
na uzito wa kilo 5.2 ambapo walifanyiwa vipimo na Padri Frolence
Mchunguzi aliyewapokea hospitalini hapo kutoka Zahanati ya Nyaruma na
kukuta uzito wao umepungua hadi kilo 3.6.
Habari zilizolifikia Uwazi wakati
linakwenda mitamboni zilieleza kwamba mzazi huyo na watoto wake walikuwa
wamehamishiwa katika Hospitali ya Bugando kwa ajili ya huduma kubwa
zaidi.
Kwa yeyote aliyeguswa na habari hii na anayetaka kuwasaidia, anaweza kuwasiliana na familia hiyo kwa namba 0787-776 123.

Note: Only a member of this blog may post a comment.