Kijana
 mmoja aitwaye Simon Dustan Mwanjavala maarufu kama Mwachakala (15) 
mkazi wa kijiji cha Mbwila kata ya Luana wilaya ya Ludewa mkoani Njombe 
amefariki dunia muda mchache baada ya kukutwa akifanya mapenzi na 
Nguruwe
Tukio
 hilo la kustaajabisha limetokea jana wilayani Ludewa baada ya kijana 
huyo "kufumaniwa" akifanya mapenzi na mnyama huyo, ndipo walipomkamata 
na kumfunga kamba mikono yake na miguu ili asikimbie
Baada
 ya majirani kumuona kijana huyo akimbaka nguruwe huyo kwenye banda la 
mnyama huyo walikwenda kumwambia baba yake mdogo ambao kwa pamoja 
walimkamata kijana huyo, ambaye alikiri kufanya kosa hilo
Alipoulizwa sababu zilizomfanya kufanya mapenzi na nguruwe, alisema alikuwa na hamu ya kufanya tendo hilo
Kutokana
 na kitendo hicho waliamua kumvua nguo zote na kumfunga kamba na kumpa 
kichapo  kisha wakamuacha kwa muda kwenye eneo la tukio, na walipokuja 
kumfungua kamba na mwenyekiti wa kijiji hicho, alidondoka na kufariki 
dunia papo hapo
 

Note: Only a member of this blog may post a comment.