
Waziri
 mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa, amesema 
hakuwa na taarifa yeyote juu ya uteuzi wake uliofanywa na Rais.
Akizungumza
 na Azam TV, Mheshimiwa Majaliwa amedai usiri uliotumika ni mkubwa ambao
 hata yeye atauendeleza katika kuimarisha Serikali.
“Huwezi amini mpaka asubuhi nafanya zoezi na Wabunge wenzangu sikuwa najua lolote, mimi ni kocha wa timu ya mpira ya Bunge.
"Yani
 mpaka Spika ameanza na ile Ruangwa nikapigwa na butwaa, na nimelia kwa 
sababu sikuamini kilichotokea, ila ndo hivyo Rais ameniamini akanipa 
nafasi” alisema Mh. Majaliwa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.