Kasi aliyoanza nayo Rais John Magufuli ya kupambana
na watumishi wasiowajibika kwenye ofisi za umma, kutoa maagizo na
kuchukua hatua mbalimbali, isitumiwe kama kipimo cha utendaji wake kwa
kuwa ni mapema, wasomi wamesema.
Kwa mujibu wa wasomi hao, muda mzuri wa kumpima ni baada ya kufikisha angalau siku 100 Ikulu. Walisema kila rais ana staili yake ya utendaji wa kazi na kwamba anaweza kuanza kwa nguvu, baadaye akapoa na anaweza kuanza taratibu na akawa moto baadaye.
Leo ni siku ya 10 tangu Dk Magufuli aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na tayari ameshatoa maagizo kadhaa likiwamo la kusitisha safari za nje za viongozi na kuagiza shughuli zote nje ya nchi zifanywe na kusimamiwa na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi hizo.
Pia, aliiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukusanya kodi kwa wafanyabiashara wakubwa bila woga, kutoa wiki moja kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuhakikisha mashine za uchunguzi za CTSCAN na MRI zinafanya kazi.
Agizo hilo lilitekeleza ndani ya siku nne tu, kwa mashine ya MRI kuanza kufanya kazi. Alipoulizwa kuhusu hatua hizo, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Richard Mbunda alisema si sahihi kuanza kumpima sasa. “Kiutamaduni muda sahihi wa kupima utendaji wazi wa mtu ni siku 100.
Hapo utaweza kuorodhesha mambo aliyoyafanya na siku 10 za Rais ni mwanzo wa kuzifikia siku 100,” alisema.
Alisema kikatiba Rais wa nchi ana jukumu kubwa, ikiwa ni pamoja na kuanzisha taasisi ambayo itasimamia mambo aliyoyaahidi au anayotaka kuyatekeleza, jambo alilodai kuwa Dk Magufuli anaweza kulifanya ili kuweza kutekeleza na kufuatilia ahadi alizozitoa kwa wananchi.
“Siasa hufananishwa na uongo na ndiyo maana mtu ukizungumza jambo fulani watu wanaweza kumwambia ‘acha siasa nyingi’, nadhani anachokifanya Dk Magufuli ni kubana matumizi ili aweze kutekeleza ahadi yake ya elimu bure.
“Nampongeza kwa kuanza kufanya mambo tofauti. Rais
(Jakaya) Kikwete wakati akiingia madarakani kuna mambo alifanya ila
hayakuwa na uzito kama haya aliyoanza nayo Magufuli,” Mbunda.
Mhadhiri mwingine wa chuo hicho, Dk Benson Bana aliungana na Mbunda, huku akisisitiza kuwa ni mapema kumpima Magufuli wakati hata baraza la mawaziri hajaunda.
Anatoa maagizo na sehemu nyingine analazimika kwenda mwenyewe ni jambo zuri. “Kwa dalili hizi za mwanzo kabisa anaonyesha kuwa amedhamiria na hasa pale alipobana matumizi ya fedha kwa kufuta safari za nje maana zilikuwa ni safari ambazo watu wanajipatia fedha kienyeji,” Bana.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ruaha, Profesa Gaudence Mpangala alisema:“Tumpe muda zaidi huu ni mwanzo tu. Kila rais ana staili yake, wapo wanaoanza kwa kusoma mazingira kwanza na kujipanga na kisha kuanza kazi na wapo wanaoanza kazi kwa kishindo.”
Alisema anachokifanya Magufuli ni kutaka kuwaonyesha Watanzania kuwa ahadi alizozitoa zinatekelezwa, kwamba hilo linaonekana kupitia mambo aliyoyafanya hadi sasa. “Binafsi, naona Magufuli anahitaji apate wataalam wa kufanya utafiti katika sekta mbalimbali.
Akipata majibu ya tafiti hizi anaweza kuzishirikisha taasisi za Serikali kufanya uamuzi wa kuleta mabadiliko,” alisema. Alisema lazima utafiti ufanyike ili kubaini tatizo la kuzorota na kusuasua kwa sekta mbalimbali nchini.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Gratian Mukoba alisema, “Siku 10 ni ndogo sasa nadhani baada ya siku 100 tutaweza kupima utendaji kazi wa rais.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.