Tuesday, November 3, 2015

Anonymous

Huenda Ukawa Hufahamu, Hii ni Rekodi ya Kuvutia ya Justice Majabvi wa SIMBA SC Katika Historia Yake ya Soka!


Justice Majabvi ni kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe ambaye anakipiga katika klabu ya Simba ya Tanzania, kiungo huyo ambaye anakipiga katika klabu ya Simba aliwahi kucheza katika vilabu kadhaa ikiwemo LASK Linz ya Australia aliyodumu nayo katika kipindi cha miaka mitatu na klabu ya Vicem Hai Phong FC ya Vietnam. 

Najua unamfahamu Justice Majabvi wa Simba hususani kwa sababu anacheza katika moja kati ya klabu kubwa Tanzania. Majabvi ana rekodi ambayo inavutia hususani kwa mchezaji ambaye amecheza kwa mafanikio katika kipindi kirefu. Licha ya kuwa Majabvi anacheza katika kikosi cha kwanza cha Simba, ila toka amejiunga na klabu hiyo hajawahi kuoneshwa kadi ya njano au nyekundu katika mechi zote hata za kirafiki.

DSC_0017
Justice Majabvi hajawahi kuoneshwa kadi nyekundu katika historia yake ya soka, Majabvi aliwahi kupata kadi za njano nyingi mwaka 2009 akiwa katika Ligi ya Australia Bundesliga ambapo alioneshwa jumla ya kadi za njano 9 katika mechi 36, mwaka 2010 Majabvi alioneshwa kadi nne za njano.
Kutokana na kadi hizo Majabvi ana wastani wa kuoneshwa kadi 2 kwa msimu, hii inaonesha ni jinsi gani Majabvi alivyokuwa na nidhamu uwanjani tofauti na wachezaji wengine ambao huchukulia pouwa kuoneshwa kadi nyekundu au njano.

IMG_20151103_000305-via millardayo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.