Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewatoa wasiwasi wananchi kwamba uchaguzi
mkuu wa madiwani, wabunge na rais unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25,
mwaka huu utakuwa wa amani.
Lubuva alitoa kauli hiyo leo katika mkutano
baina ya tume hiyo na wahariri wa vyombo mbalimbali ambao umefanyika
kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.Akizungumza huku akiwa
sambamba na makamishna wa tume hiyo, Lubuva alisema tume yake imejiandaa
vizuri kwa uchaguzi huo.
“Mtu au chama chochote kisihofu kuhusu
uchaguzi kwani utakuwa wa amani na utulivu kwa nchi nzima, kwani imeweka
mazingira mazuri kwa wananchi kupiga kura bila tatizo,” alisema Lubuva.
Aidha, mwenyekiti huyo ametoa rai kwa wananchi mara wakimaliza zoezi
la kupiga kura warudi majumbani mwao kusubiri matokeo kutangazwa na
mamlaka husika.
(HARUNI SANCHAWA WA GPL)
Note: Only a member of this blog may post a comment.