Monday, October 5, 2015

Anonymous

Wagombea wa Mwaka Huu Wote Wababaishaji! -WITNESS

Rapper Witness amesema hatopiga kura katika uchaguzi mkuu mwaka huu kutokana na wagombea mbalimbali kushindwa kuzungumzia vitu vya msingi kwenye kampeni zao.
Witness aliiambia Bongo5 kuwa haoni thamani ya kura yake tena.
“Ni haki ya kila mtanzania lakini kama sioni mabadiliko yoyote nipige kura ya nini? 
Kwa sababu toka nimezaliwa kuna maisha nayoishi ambayo sipendi kuishi, siwezi kupiga kura kwa sababu wagombea hawazungumzi vitu vya msingi. Watu tuna matatizo, maisha magumu, vitu vinapanda bei kila siku, hivi vitu hawavizungumzii. Mimi naona bado kura yangu itawasaidia wao kula vizuri, kuishi vizuri pamoja na kuwasafirisha kwenda nje. Mimi pia nataka kula vizuri na kusafiri kwenda nje ,” alisema Witness.

Aliongeza, “Mimi sionekani kwenye majukwaa ya siasa kwa sababu zamani tuliambiwa, siasa na sanaa ni vitu viwili tofauti na mimi ndio nimekuwa na msimamo huo. Lakini kama kukitokea show ya kampeni nafanya kama biashara, mimi nafanya biashara ya muziki siwezi kukataa.” 

-via Bongo5

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.