Edward Lowassa
Na Mwandishi Wetu
MTABIRI maarufu
nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein, amesema utabiri wake alioutoa
mwaka 2014 kwamba mgombea urais mmoja atafariki dunia ghafla kabla ya
uchaguzi, umetimia baada ya kifo cha Mchungaji Christopher Mtikila na
kuwaacha salama wagombea Edward Lowassa na Dk. John Magufuli.
Maalim Hassan aliyasema hayo
alipozungumza na gazeti hili juzi ambapo alisisitiza kuwa utabiri wake
alioutoa Desemba 28, 2014 katika mkutano wake na waandishi wa habari
ofisini kwake, haukumlenga mtu.
Mchungaji Mtikila ambaye alikuwa
akigombea urais kupitia Democratic Party (DP) kabla ya kuenguliwa na
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), alifariki dunia Oktoba 4, 2015 kwa
ajali ya gari kijijini Msolwa, Chalinze, mkoani Pwani akitokea Njombe.
“Nilipoutoa utabiri ule mengi yalisema
na watu wakawataja wagombea fulani, lakini niliwaambia kwamba utabiri
haulengi mtu na sasa umempata Mchungaji Mtikila.
“Mtikila alikuwa mgombea urais,
alichukua fomu na watu wakaona akiwa na mkoba kama wa wagombea wenzake,
akakataliwa na tume lakini akakata rufaa… angeweza pia kushinda rufaa
yake,” alisema Maalim Hassan.
Aliongeza kuwa, mara baada ya utabiri
wake alipigiwa simu na makada wa vyama viwili – Chama cha Mapinduzi
(CCM) waliodai kuwa mgombea wao Dk. Magufuli haumhusu na wale wa
Chadema nao wakasema mgombea wao, Lowassa hawezi kuchuliwa hivyo –
akawajibu wote kwamba utabiri wake haumlengi mtu.
“Niwahakikishie wananchi kwamba, kinyota
wagombea wote wa urais waliobaki sasa wako salama na watashiriki
kuchagua viongozi Oktoba 25, mwaka huu,” alisema Maalim Hassan.
Note: Only a member of this blog may post a comment.