Na Makongoro Oging’
HALI tete! Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke,
Dar lilifanikiwa kumdhibiti mtu mmoja ambaye jina lake halikupatikana
mara moja kufuatia madai ya kuvamia Kituo cha Polisi Charambe akiwa na
panga.
Habari zilizopatikana kutoka kwa raia wa eneo hilo ambao walimtafsiri
mtu huyo kama gaidi kutokana na ujasiri wake wa kuvamia kituo kwa
mapanga kwa lengo la kutaka kuwajeruhi askari kituoni hapo bila uoga.
Uwazi
ambalo lilifika kituoni hapo mara baada ya tukio hilo, liliambiwa
kwamba mtu huyo alijitokeza kituoni hapo majira ya saa sita mchana na
kuanza kuwapiga polisi na ubapa wa panga hali iliyozua tafrani.
Wananchi hao kwa nyakati tofauti walisema kwamba, mtu huyo alikuwa na
nguvu nyingi kiasi cha kuwafanya askari kuchukua muda mrefu kumdhibiti
kwani hapa kumpiga pingu ilikuwa shughuli pevu.
Taarifa
zaidi toka kwa wananchi hao zinadai kwamba, ili askari waweze
kumdhibiti ilibidi afungwe pingu haraka. Hata hivyo, licha ya kujeruhiwa
miguu bado alikuwa akiongea kwa sauti ya juu nje ya kituo hicho,
akiwalaani askari hali iliyowafanya wananchi kuzidi kujaa huku wakidai
si mtu wa kawaida.
Vyanzo
vingine makini vilidai kwamba, kutokana na hali iliyojitokeza kwa mtu
huyo kutotii amri ya polisi iliwafanya askari waongezeke baada ya
kupigiwa simu kwa hofu kuwa huenda ana wafuasi wake ambao wangeweza
kuvamia kituo wakati wowote.
Vyanzao hivyo viliendelea kudai kwamba zaidi ya difenda tatu ambazo
zilikuwa na polisi zilifika kituoni hapo muda mfupi baadaye na kila
askari alionekana akiwa tayari kwa lolote.
Ilidaiwa kwamba hali hiyo ilimfanya Kamanda wa Polisi Temeke, ACP Andrew Satta kufika ili kushuhudia hali hiyo kwa macho.
Baadhi ya wananchi walisema mtu huyo alikuwa na wenzake ambao
haikujulikana walikoelekea na ndiyo sababu polisi walipatwa na hofu. Mtu
huyo alichukuliwa hadi Kituo cha Polisi Mbagala kwa mahojiano zaidi.
Kamanda Satta alipohojiwa na Uwazi kwa njia ya simu alisema hayupo
ofisini hivyo alimtaka mwandishi kufika ofisini kwake. Mwandishi
alipofika hakumkuta ofisini na simu yake ilipopigwa ilikuwa ikiita bila
kupokelewa.
Bado gazeti hili linaendelea kufuatilia suala hilo kwa karibu ili kujua ni kitu gani kilitokea. Endelea kutembelea mtandao huu wa kandiliyetu.com
Note: Only a member of this blog may post a comment.