Thursday, October 8, 2015

Anonymous

USIPITWE! Mzee KINGUNGE Kumnadi LOWASSA Jijini Arusha Leo...Aomba Dakika 40 za Kuichana CCM

Mwanasiasa mkongwe na mmoja kati ya waasisi wa Tanu na CCM aliyetangaza kuachana na chama hicho hivi karibuni, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amepanga kupanda rasmi kwenye jukwaa la Ukawa, leo jijini Arusha kumnadi mgombea wa Chadema, Edward Lowassa.

Taarifa za Kingunge kumnadi rasmi Lowassa leo, zimethibitishwa na meneja wa kampeni wa Chadema, John Mrema.
“Kesho (Leo) Kingunge atangumza na watanzania kueleza kile anachokiamini, anataka mabadiliko, cha muhimu ni ujumbe wake,” Mrema alikaririwa jana.
Mzee Kingunge alitangaza kuachana na CCM kwa madai kuwa chama hicho kimepoteza mwelekeo.
Alisema utaratibu uliotumiwa kumpata mgombea Urais wa chama hicho kupitia vikao vya kamati ya maadaili na usalama vilienda kinyume na taratibu na katiba ya chama hicho kwa maslahi ya viongozi wachache.

Mwanasiasa huyo mkongwe alisema hatajiunga na chama chochote cha siasa kwa sasa lakini atabaki kuwa upande wa wale wanaotaka mabadiliko ya kuiondoa madarakani serikali ya CCM

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.