UCHAGUZI MKUU 2015: Hemedy PHD Ana Pointi Muhimu Sana Hapa!
Hemed Suleiman ‘Phd’ ametoa rai kwa masanii wenzake kutoa elimu juu ya upigaji kura katika Uchaguzi Mkuu wa baadaye mwezi huu badala ya wenyewe kuwa mashabiki wa vyama.
Pamekuwa na wimbi kubwa la wasanii tukumika kisiasa katika kipindi hiki cha kampeni kwa kinachodaiwa kuwa malipo makubwa hasa kutoka CCM.
Lakini badala ya kupanda kwenye majukwaa na kupigia kampeni upande mmoja katika uchaguzi huo, Phd ametaka watoe elimu ya upigaji kura.
Alisema asilimia kubwa ya wapiga kura mwaka huu ni wageni katika maswala ya upigaji kura , hivyo wanahitaji elimu ya kutosha.
“Nashangaa wasanii wenzangu badala ya kusimamia kwenye maswala ya upigaji kura, wao wamekuwa wa kwanza kutukna wagombea”, alisema.
Chanzo: Lete Raha
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Note: Only a member of this blog may post a comment.