Saturday, October 3, 2015

Anonymous

SIRI IMEFICHUKA! Watangazaji wa BSS 2015...PENNY, SIZA Wanaswa Kimahaba Hadharani!

Imelda Mtema
WATANGAZAJI wa Shindano la Bongo Star Search, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Siza Daniel wamenaswa wakioneshana mahaba hadharani kama mtu na ‘bebi’ wake.
Tukio hilo lililopigwa chabo na paparazi wetu lilijiri wikiendi iliyopita maeneo ya Kawe Beach, Dar wakati wawili hao walipokuwa wakijiandaa kurekodi kipindi cha shindano hilo ambapo walionekana kushea juisi ambayo kuna wakati Siza alimnywesha Penny huku wakati mwingine, Penny akijibu mapigo.
Wawili hao baada ya kupigwa picha na paparazi wetu na kuwauliza kama ni wapenzi, Siza alishindwa kuzungumza lolote lakini Penny alipoulizwa kama jamaa huyo ndiye mrithi wa Diamond (Nasibu Abdul), alijibu kwa kifupi:
“Jamani kusoma hujui hata picha huoni?”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.