Monday, October 26, 2015

Anonymous

RASMI: Historia Yawekwa TARIME, Mara...ESTHER MATIKO wa CHADEMA Ashinda Ubunge!

Haijawahi kutokea mkoa wa Mara ukaongozwa na mwanamke kwa kuchaguliwa kupitia sanduku la kura lakini kwa mara ya kwanza hivi punde ESTER MATIKO wa Chadema ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo! 
MATOKEO YAPO HIVI
Esther Matiko amepata kura 20,017 na kumshinda mpinzani wake wa karibu Kembaki Michael Mwita wa CCM aliyepata kura 14,025.
 
Tunaisubiri taarifa rasmi toka Bunda ambapo mwanamke mwingine Ester Bulaya anagombea ubunge ingawa taarifa za awali zinaarifu mgombea huyu kambwaga mzee Wassira!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.