#UCHAGUZI2015: Jeshi la Polisi limekita kambi Temeke mikoroshini kata ya Sandali jimbo la Temeke baada ya hali kuelezwa kuonekana tofauti kutokana na vijana wa eneo hilo kujaa kwa wingi kwa kile kinachoelezwa wanataka matokeo yatangazwe kwani wana wasi wasi na utangazwaji wa matokeo.
Wananchi hao wanadai kuwa wana wasiwasi kutangazwa matokeo tofauti wakati wanaamini mgombea wao kutoka CUF atakuwa kashinda dhidi ya CCM,lakini bado mawakala hawajaweka wazi matokeo hivyo hadi sasa.
Kwa Mujibu wa muandishi wetu Sam Mahela aliyepo eneo hilo anayefuatilia taarifa hizi za uchaguzi anasema kuwa licha ya jeshi la polisi kuwepo eneo hilo linahakikisha hakuna tatizo lolote linalo tokea na kuona wasimamizi wakitangaza matokeo bila hofu.
Ungana nasi kwa kila hatua katika taarifa hizi za Uchaguzi,ITV/Radio One na Capital Radio.
Wananchi hao wanadai kuwa wana wasiwasi kutangazwa matokeo tofauti wakati wanaamini mgombea wao kutoka CUF atakuwa kashinda dhidi ya CCM,lakini bado mawakala hawajaweka wazi matokeo hivyo hadi sasa.
Ungana nasi kwa kila hatua katika taarifa hizi za Uchaguzi,ITV/Radio One na Capital Radio.

Note: Only a member of this blog may post a comment.