Kufuatia Kazi Nzuri Iliyotuka Inayofanywa na ITV, Mnaonaje Mzee MENGI Akabidhiwe Kuiendesha TBC?
Kufuatia Kazi Nzuri na Iliyotuka Inayofanywa na vyombo vya habari vya
IPP, in particular, kituo cha televisheni cha ITV, katika uchaguzi huu,
Jee Mnaonaje Kama tukiishauri serikali ijayo, imkabidhi Mzee Reginald
Mengi, Jukumu zito la Kuiendesha TBC?!.
Najua wazo langu hili litapata upinzani, toka kwa watu wanaojiita
wazalendo, kwa kuleta hoja, huwezi kuibinafsisha TBC kwa sababu ni
taasisi nyeti!. Hili sio jambo la ajabu, Tanzania tumeisha binafsisha
taasisi mbalimbali na nyingine ni nyeti zaidi ya TBC mfano, City Water,
TTCL, Tanesco, TRL, ATC etc.
Swali hili ni kufutia ITV kuwa ndio tegemeo pekee la taarifa za matokeo
ya Uchaguzi Mkuu, as if ITV ndio TV ya Taifa, jukumu ambalo lingepaswa
kubebwa na TBC!. Kama hoja ni uzalendo, ni nani mzalendo halisi wa taifa
hili kati ya ITV na TBC?!.
Hongera sana ITV, Hongera Mzee wetu, Reginald Abraham Mengi, hongera
menejiment ya ITV ikiongozwa na Iron Lady, Joyce Mhavile, na Hongera kwa
News team yote ya ITV ambayo ni hakuna kulala, mnafanya kazi 24/7,
hivyo na sisi huku majumbani mwetu, tunakesha na nyinyi!.
Mungu awabariki sana!.
Maoni Huru Kutoka Kwa Pasco /Jamii Forums
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Note: Only a member of this blog may post a comment.