Adam Malima ‘kushoto’ akimpigia kampeni Abdalah Ulega anayegombea Jimbo la Mkuranga badala yake.
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Pombe Joseph Magufuli jana aliendelea na mikutano ya kampeni zake mkoani Lindi katika maeneo ya Kijiji cha Nangaru, Jimbo la Mchinga, Mavuji, Kilwa Masoko na Marendego.
Baada ya kumaliza kampeni mkoani Lindi, Magufuli aliingia Mkoa wa Pwani ambapo alipiga kampeni katika maeneo ya Nyamwage, Ikwiriri, Kibiti, Jaribu, Kimanzichana, na kumalizia na Mkuranga ambapo mkutano huo ulihudhuliwa na umati mkubwa na kuvunja rekodi ya siku nzima licha ya mikutano iliyotangulia nayo kuhudhiliwa na maelfu ya watu.
Magufuli leo anatarajiwa kujiunga na Watanzania wengine kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere, Dar kuupokea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Abdallah Kigoda, aliyefariki nchini India juzi alikokuwa ameenda kutibiwa, kabla ya kesho kuendelea na kampeni.
Note: Only a member of this blog may post a comment.