Wednesday, October 14, 2015

Anonymous

PICHAZ: Jeuri ya Pesa! Shuhudia Floyd Mayweather Akienjoy na Rafiki Zake Huko Miami!


Bondia mwenye rekodi ya kutopigwa Floyd Mayweather bado anaendelea kufanya matanuzi ya mkwanja wake aliyovuna katika mchezo wa ngumi. Floyd Mayweather ambaye mwezi September alimpiga kwa point bondia Andre Berto pambano lililofanyika katika ukumbi wa MGM Grand Garden Arena Las Vegas Marekani.

Mayweather Jr alipigwa picha akiwa katika bwawa la kuogelea Miami sambamba na uwepo wa rafiki zake, huku akionekana kujiachia zaidi dalili ambazo zinaashiria kuwa hana pambano hivi karibuni kwani muda mwingi ameonekana akiwa anaenjoy na rafiki zake.
Bingwa huyo wa uzito wa kati hadi sasa ana rekodi ya kupigana mapambano 49 na kutopoteza pambano hata moja kati ya hayo. Hata hivyo kuna stori zinazozungumzwa kuhusu promota maarufu wa mchezo wa ngumi Bob Arum kutaka kuandaa pambano la marudiano kati ya Mayweather Jr dhidi ya mpinzani wake Manny Pacquiao.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.