Chanzo cha habari kilicho karibu na timu ya kampeni ya CCM, kimesema
chama chao ndiyo kama kinaanza rasmi shughuli hiyo leo, kwani
kinategemewa kuanza kutumia ‘silaha’ nzito ili kuhakikisha
kinausambaratisha upinzani.
“Jamaa
wana helikopta zipatazo tano ambazo zimegawanywa kwa wana kamati
kushambulia maeneo mengi kadiri wanavyoweza, lengo ni kuyafikia maeneo
ya ndani na ambayo kidogo yanakuwa vigumu kupitika kwa njia ya barabara,
katika siku hizi zilizobaki, kila eneo litafikiwa,” kilisema chanzo
hicho.
Wakati kukiwa na taarifa hizo kutoka chama tawala, Ukawa nao
wanasemekana kuandaa ‘majeshi’ yao ya maangamizi kwa kutumia jumla ya
helikopta saba ambazo zitaanza kazi ya anga kwa anga ili kuwafikia
wapiga kura katika hatua hii ya lala salama.
“Ni kweli, zimetayarishwa helikopta saba zitakazoanza zoezi kali la
kutafuta kura katika hatua za lala salama, Hizi zimegawanywa kwa
makamanda tofauti wa kuongoza mapambano, nina uhakika Lema (Godbless,
Arusha) atakuwa nayo moja, Wenje (Ezekiel, Nyamagana), Msigwa (Mchungaji
Peter, Iringa), Lissu (Tundu, Singida) kila mmoja atakuwa na chopa ya
‘kumwaga sumu’ kila kona ya Tanzania,” alisema kiongozi mmoja wa umoja
huo, aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa siyo msemaji.
Note: Only a member of this blog may post a comment.