OHOOO! Kuna
madai kwamba, ile pati ya kukata na shoka ya kutimiza siku 40 kwa mtoto
wa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Latifah Nasibu
‘Princess Tiffah’ iliisha huku nyuma ikiacha madeni ya kiasi cha
shilingi 1,005,000, Amani limechimbua.
Ni siku ya 11 sasa, kampuni iliyopewa
tenda ya kupamba kwenye shughuli hiyo iliyofanyika nyumbani kwa staa
huyo, Tegeta-Madale, Dar ya Rachel Decorations imejipambanua kuwa,
inamdai baba Tiffah kiasi hicho cha fedha na hakuna matumaini ya
kulipwa.
MENEJA WA KAMPUNI AZUNGUMZA
Akizungumza na Amani, meneja
wa kampuni hiyo ya mapambo aliyejitaja kwa jina moja la Lutengano
akisema linatosha, alisema wiki moja kabla ya sherehe hiyo iliyokuwa na
mbwembewe nyingi, dada wa Diamond, Esma Platnumz alimtafuta mpambaji
huyo na kumwambia kuwa, kuna tenda.
“Bosi wangu anaitwa Rachel, ndiye
aliyekutana na Esma wakakubaliana kisha wakaenda kwa Diamond kwa ajili
ya makubaliano ya kifedha lakini bajeti ilikataliwa baada ya kuonekana
ndogo na baadaye wakaafikiana kwamba, afanye kazi kutokana na kiasi cha
fedha alichoahidi.
DIAMOND AINGILIA KAZI ZA WATU
“Siku moja kabla ya tukio (Jumamosi),
usiku tulikwenda nyumbani kwa Diamond (Madale) na vifaa vyetu kwa ajili
ya kuanza kazi kwa kuwa shughuli ilitakiwa kufanyika asubuhi lakini
tukiwa katika maandalizi ya kufunga matenti (turubali), Diamond aliingia
na baadaye akatoka, akaanza kuelekeza anavyotaka kupambwe.
“Tulimweleza kwamba haiwezekani kutokana
na fedha ndogo waliyokuwa wametoa, akaahidi kwamba yuko tayari kuongeza
fedha ilimradi mapambo yaenee kama anavyotaka na kusema kuwa ana watu
wa muhimu watakaofika hapo hivyo panatakiwa pawe na hadhi zao. Ikabidi
tuanze kuchukua vipimo upya,” alisema meneja huyo.
MAKUBALIANO MAPYA
Lutengano aliendelea kuliambia Amani
kuwa, ilibidi wakubaliane na Diamond upya, kwamba kama anataka kuongeza
sehemu ya mapambo basi gharama ilibidi iongezeke, akakubaliana na vyote
na kutoa fedha kiasi kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo huku akisema
fedha iliyobaki angetoa siku ya sherehe huku akisema kuwa, mwandani
wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ alipendelea zaidi makapeti na
mito siyo viti kama ilivyokuwa mwanzo.
“Tukawa tumekubaliana aongeze shilingi
milioni 1,600,000 kwa sababu kulikuwa na vitu ambavyo vilitakiwa
kununuliwa, Diamond alitoa shilingi moilioni 1,300,000 na kubakisha
shilingi laki 300,000 lakini pia kabla ya hapo alikuwa akidaiwa shilingi
laki 625,000 kama fedha ya matenti 5 ambapo kila tenti liligharimu
shilingi 125,000.
“Baada ya matenti yote kufungwa,
tukasitisha zoezi la mapambo kuendelea na mimi siku hiyo sikulala,
nikaanza kushughulikia makapeti ambayo Diamond aliagiza mpaka nikaja
kuyapata muda ulikuwa umeshakwenda na hilo tulishakubaliana kwamba
kunaweza kutokea tukacheelewa kwa sababu ya muda kuwa mbaya akasema yeye
anataka iwe hivyo alivyopanga.
Lutengano anasema baada ya kuzunguka
sana Kariakoo, alifanikiwa kupata makapeti aliyoagizwa na kuyapakia
kwenye gari la mizigo kisha kuagiza gari liende Madale huku yeye
akiendelea kutafuta mito na maua.
“Kutokana na muda ulivyokuwa umekwenda
gari lilifika Madale saa 3:00 asubuhi na wenyeji wakawa wamesusa kwamba
vitu vimechelewa, vitu vikashushwa ikabidi tena mimi nianze kuwaelewesha
kwa njia ya simu namna ambavyo tulikubaliana na Diamond mwenyewe na
baadaye vitu vikaandaliwa na sherehe ikaanza.
“Kwa kuwa mimi nilikuwa nimechoka, ule
muda ambao sasa mtoto ndiyo alikuwa anatolewa ndani, ikabidi niende
kwenye gari langu nikapumzike ili nisubiri sherehe ikiisha nikaonane na
Diamond ili animalizie fedha yangu iliyobaki ambapo shilingi 625,000 ya
matenti, 300,000 ya deni la awali na 80,000 ya usafiri ambapo jumla ni
shilingi 1,005,000.”
MAMA DIAMOND AFUATWA, ASEMA NIVYO SIVYO
“Nikawa namfuata mama Diamond
kumuulizia, akanijibu hovyo kwamba tumewachefua sana, Esma naye akawa
anatukimbia. Nikawaambia watu wangu tuondoke.
“Siku iliyofuata (Jumatatu) asubuhi
nilirudi tena, nikaambiwa Diamond amesafiri. Cha ajabu mama yake
akaniambia hakuna tunachodai na yale makapeti alinunua mwanaye.
ASHINDA NJE KWA DIAMOND
“Nilikaa pale nje kuanzia saa nne
asubuhi mpaka saa tisa alasiri. Nikamwambia amuulize mwanaye kwenye simu
ili nijue nini kinandelea, Diamond akajibu kwa kifupi tena kwa kutuma
meseji kwamba si kwa upambaji ule na kusema kuwa, fedha aliyotupatia
anaona inatosha.
“Mimi nilisema lazima nilipwe fedha
zangu, Esma na mama yake wakaniambia mimi ndiye niwe ninakumbusha mara
kwa mara, Diamond ni msahaulifu sana. Niliondoka, baadaye nilimtafuta
meneja wa Diamond (Hamisi Tale ‘Babu Tale’) kwa sababu
Diamond alikuwa
hapokei simu yangu,” alisema Lutengano.
Meneja huyo aliendelea kusema kuwa, Babu
Tale alimjibu yuko bize na bethidei ya mwanaye lakini baada ya siku
chache alimuita akamwambia ameongea na Diamond akamwambia amemlipa fedha
mara mbili lakini hajaridhika na upambaji wao na fedha aliyoitoa anaona
imetosha hivyo hawezi kulipa zaidi (licha ya makubaliano).
MAMA DIAMOND ASAKWA
Kwa upande wake, mama Diamond, Sanura
Kassim ‘Sandra’ alipotafutwa na kuulizwa kuhusu madai hayo, alijibu
kifupi: “Hatudaiwi chochote waulize haohao waliokupa taarifa na namba
zangu (akamalizia na tusi).”
SIMU YA DIAMOND HAIPOKELEWI
Simu ya Diamond ilipopigwa haikupatikana hewani muda wote, lakini Babu Tale yeye alisema hajui lolote kuhusu mapambo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.