Rapper Mr Blue amesema kuingia kwenye uvutaji wa bangi kulimsabisha aache shule na kutaka kukaa kijiweni zaidi.
Mr Blue aliliambia gazeti la Mwananchi kuwa, kuna vitu vingi ameshindwa kufanya kotokana na kuwa mtumwa wa bangi.
“Najuta kujiingiza kwenye matumizi ya bangi,” anasema. “Siwezi kusema
ni madawa ya kulevya kama inavyojulikana kwa unga na cocaine. Sijawahi
kufikia huko, bali nilivuta sana bangi na pombe kali ila kwa sasa
nimeacha kabisa.”
“Mambo mengi kwenye maisha yangu yalikuwa hayafanyiki kadri
nilivyokuwa nataka, nilikuwa napoteza muda wangu kwenye kukaa kijiweni
kuliko kufanya kazi,” alimalizia Blue.
Note: Only a member of this blog may post a comment.