Waziri wa viwanda na Biashara, Abdalah Kigoda (Mb) enzi za uhai wake.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Abdalah Kigoda amefariki dunia
majira ya saa kumi jioni ya leo katika hospitali ya Appolo nchini India
alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungao wa Tanzania kupitia kitengo cha
Habari, Elimu na Mawasiliano imekili kupokea taarifa za msiba huo jioni
ya leo na kusema kuwa, taarifa zaidi kuhusu taratibu za kuusafisha mwili
wa marehemu kutoka India kuja hapa nchini na mipango ya mazishi
zitaendelea kutolewa na serikali pamoja na Ofisi ya Bunge kwa
ushirikiano na familia kadri zitakavyokua zinaendelea kupatikana.
“Inna Lillahi wa inna ilaihi raji’un”
Note: Only a member of this blog may post a comment.