Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha.
Brighton Masalu
Siku chache baada ya mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha kufuta kesi ya kudai talaka mahakamani na kudai kuwa bado ana ‘mapenzi’ na mumewe, Emmanuel Mbasha ameibuka na kujiapiza kuwa kutokana na ukali wa mateso aliyoyapitia wakati wa kesi yake, kamwe hawezi kumsamehe mwanamke huyo.
Siku chache baada ya mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha kufuta kesi ya kudai talaka mahakamani na kudai kuwa bado ana ‘mapenzi’ na mumewe, Emmanuel Mbasha ameibuka na kujiapiza kuwa kutokana na ukali wa mateso aliyoyapitia wakati wa kesi yake, kamwe hawezi kumsamehe mwanamke huyo.
Akizungumza na Ijumaa kwa njia ya simu,
Jumatano ya wiki hii siku moja baada ya Flora kuamua kufuta kesi hiyo
katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar, Mbasha alilalamikia yale
aliyofanyiwa na mwenza wake huyo kipindi cha nyuma kiasi cha kutoona
sababu ya kurudiana naye.
MSIKILIZE KIDOGO MBASHA
“Flora ni mwanamke muongo na mnyama, anawezaje kujitokeza hadharani
kipindi hiki na kudai kuwa amefuta kesi ya talaka na kwamba ananipenda,
kweli? Ni wiki mbili tu zilizopita nilikuwa hatarini kwenda jela kwa
zaidi ya miaka 30, alikuwa wapi kuja kunitetea na kufuta kesi hiyo?
Alikuwa wapi huyu?
“Kaniharibia kila kitu, maisha yangu
yaliyumba kwa kuwazia kesi ya kusingiziwa kubaka, kama siku ya kesi pale
mahakama ya Ilala ningefungwa, leo hii angeyasema hayo?
HATAKI HATA KUMUONA!
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, licha ya kuwa ni mzazi mwenzake,
Mbasha alisema hataki hata kumuona Flora kwa kile alichokiita “kukaa
mbali na wakala wa shetani” na kwamba kamwe hawezi kumsamehe.
“Kaka, afanye maisha yake, sitaki hata kumona na kamwe siwezi kumsamehe Flora kabisa, never (kamwe),” alisema Mbasha.
TUJIKUMBUSHE NYUMA
Mnamo Septemba 21, mwaka huu Mbasha aliachiwa huru dhidi ya madai ya
kesi iliyokuwa ikimkabili ya kumbaka shemeji yake, katika Mahakama ya
Ilala, jijini Dar ambapo Jumanne ya wiki hii alifikishwa tena katika
Mahakama ya Kisutu jijini Dar na Flora akimdai talaka.

Note: Only a member of this blog may post a comment.