Mwandishi wetu, Mwanza
MAUZAUZA! Mwanamke mmoja mtu mzima, ambaye jina lake
halikufahamika mara moja amekutwa akiwa ndani ya nyumba ya mtu pasipo
kueleweka namna alivyoingia, kwani milango yote ilikuwa imefungwa kwa
ndani.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni majira saa 2 asubuhi maeneo ya Majengo, wilayani Misungwi, mkoani Mwanza na kujaza watu wengi.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni majira saa 2 asubuhi maeneo ya Majengo, wilayani Misungwi, mkoani Mwanza na kujaza watu wengi.
“Baada ya kumkimbiza na kumkamata, tulimuweka chini ya ulinzi na
kumhoji, akashindwa kujieleza kwa usahihi, tukaamua kumuachia aende
zake, lakini kuna baadhi ya watu hawakuridhika, wakaendelea kumhoji,
ndipo akatoa hirizi na pasipoti za watu ambazo hakusema anazitumia kwa
mambo gani,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
“Wakati naendelea kupiga kelele nikakumbuka mwanangu nimemuacha ndani
amelala, nikarudi maana nilihisi angemdhuru, wakati nafungua mlango
yule bibi alitoka nduki hapohapo watu waliokuwa wamekusanyika nje
walianza kumkimbiza.”
Dawa alizokutwa nazo baada ya kupekuliwa.
Alisema baada ya kubanwa na kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha juu
ya picha na madawa na hirizi aliyokutwa nayo, wananchi hao waliamua
kuita polisi ambao walimpeleka kituo cha Polisi Misungwi kwa mahojiano
zaidi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.