Alhaj Ahamed (kafa).
Na Makongoro Oging’
Baadhi ya wananchi ambao ndugu zao
walikwenda kuhiji mjini Mina, Maka, Saudi Arabia, wana hofu kwa kuwa
asilimia kubwa bado hawajarejea nchini huku wengine wakitajwa wamefariki
dunia.
Hajat Khadija (kafa).
Wananchi hao waliohojiwa na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita,
kwa nyakati tofauti walisema ni mahujaji wachache waliorejea, wengine
wamefariki dunia na kuzikwa huko na baadhi hawajaonekana kabisa huku
kukiwa na taarifa kuwa wapo wanaotarajiwa kurudi hivi karibuni.
Alhaj Athuman (kafa).
Hata hivyo, mwandishi wetu alikwenda
ofisi ya taasisi mojawapo inayosafirisha mahujaji ijulikanayo kwa jina
la Ahlu Daawa Hajj iliyopo Magomeni jijini Dar na kukutana na mmoja wa
viongozi, Ustadhi Yusuph Mohamed ambaye alikuwa na haya ya kusema:
Hajat Fatia (hajarudi).
“Ni kweli tumepokea taarifa ya vifo vya mahujaji na kuna wengine
wanaendelea na matibabu huko huku baadhi yao wamesharudi na wapo ambao
tunatarajia kuwapokea Oktoba 10, mwaka huu, najua kila mmoja anajua
kilichotokea huko, mahujaji wengine bado hawajulikani walipo.
Hajat Zuhura (hajarudi).
“Tutaendelea kutoa taarifa kadiri
tunavyopata habari kwani tumekuwa tukiwasiliana na uongozi wa taasisi
hii ambao wako huko Maka na tuna ushirikiano na ubalozi wetu wa huko na
Wizara ya Mambo ya Nje ya hapa kwetu ambao wamekuwa nasi bega kwa bega
kufuatilia suala hili,” alisema Ustaadhi Mohamed.
Alhaj Shafii (kafa).
Aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Seif Salum Kitimla, Shafi Ally,
Hadija Shekari Mohamed wote wa Dar, Ahamed Said Bawazili waTanga na
Athumani Mateso Chaulana wa Pwani.
Hajat Joha (hajarudi)
Aliwataja mahujaji waliorudi, walipotoka kwenye mabano kuwa ni Salama
Jumbe Mkumbo (Pwani), Badilu Abdallah Kiboko (Bukoba), Abdallah Mwidadi
Kuluvya (Tanga), Seleman Salum Said (Pemba), Rehema Salehe Mbaraka
(Tanga), Ramadhani Sharia Amir (Dar).
Aliwataja wengine kuwa ni Issa Ibrahim Magoye (Mpanda), Mohamed Seif
Kiukala (Pwani), Fatina Mohamed Said (Dar), Haruna Yahaya Kiyekumbya
(Karagwe), Mohamed Issa Kidomi (Dodoma), Mwanamkuu Mohamed Ahmed (Tanga)
na Abdallah Mohamed Al Lawii (Zanzibar).
Alisema ambao bado hawajarudi ni pamoja na Hawesu Mashaka Mwinyimkuu
(Dar), Idd Musa Kibadeni (Tabora), Masibu Mohamed Fikirini (Morogoro),
Fatia Mohamed Karim (Tanga), Zuhura Toba Waziri (Tanga).
Wengine ambao hawajarudi ni Hirari Hamis Salum (Bukoba), Salim
Nassoro Salim (Pemba), Joha Salim Baraka (Tanga), Sophia Abdallah Msindo
(Tanga), Karim Fatia Ali (Pemba) na Siwatu Misho Mwishehe (Dar).
Note: Only a member of this blog may post a comment.