Sunday, October 4, 2015

Anonymous

MAGUFULI Azidi Kuchanja Mbuga, Awaomba Wana CHADEMA Waichague CCM

Magufuli akiwasalimia wanachadema wa Manyoni na kuwataka wampigie kura yeye na mbunge wake Daniel Mutuka.

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) John Magufuli, jana alimwaga sera katika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma na kuingia Mkoa wa Singida ambapo alifanya mikutano kwenye vijiji miji ya Chikuyu, Kilimatinde, Manyoni, Itigi, na kumalizia na Itigi iliyopo Jimbo la Singida Mashariki.
Katika mikutano hiyo Magufuli aliitangaza ilani ya utekelezaji ya chama chake ambayo inatoa kipaumbele kwa mambo kadhaa ikiwemo kupunguza shida ya maji safi na salama, huduma za afya, barabara, kupunguza ushuru kwa wafanyabiashara wadogowadogo na wakubwa, kutoa mikopo kwa ajili ya mitaji, elimu bure na mengine mengi.

Akimwaga sera hizo Magufuli alitoa ufafanuzi wa jinsi atakavyoiteleza ilani hiyo,hali iliyosababisha kila alipotoa ufafanuzi watu wamshangilie kwa vifijo na nderemo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.