Makocha 20 ambao ni professional wa masuala ya soka Brazil wamekutana na kupiga Kura ya kumchagua nani mchezaji bora wa soka kati ya Lionel Messi, raia wa Argentina anayekipiga katika klabu ya Barcelona, na Cristiano Ronaldo raia wa Ureno anayekipiga klabu ya Real Madrid ya Hispania.
Lionel Messi na Cristiano Ronaldo
Kati ya Kura hizo 20, Messi alipata Kura 14, huku Ronaldo akipata Kura 5 na Kura moja ilibaki wazi baada ya Kocha mmoja kushindwa kuamua Kura yake ampe nani !!
Messi anaendelea kukaa benchi la Barcelona akitibiwa jeraha la mguu, lakini kuna stori pia ya kesi inayohusu madeni ya Kodi inayomkabili baba yake mzazi wakati akiwa Hispania, vitu ambavyo huenda vinamchanganya zaidi kwa sasa.
Note: Only a member of this blog may post a comment.