Klabu ya Liverpool ya Uingereza Jumapili ya October 4 inacheza mchezo wake wa nane wa Ligi Kuu Uingereza dhidi ya Everton, mechi ambayo ni kubwa katika jiji la Liverpool kwani inazikutanisha timu zenye upinzani mkubwa kutoka mji mmoja, inatajwa kuwa mechi hiyo huenda ikaamua hatma ya kocha wa Liverpool Brendan Rodgers.
Liverpool itashuka katika uwanja wa Goodison Park
wenye uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya 30000 ikiwa na rekodi ya
kucheza mechi saba, imeshinda 3, imetoka sare 2 na kufungwa 2 na ipo
nafasi ya 9 katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza msimu huu, rekodi hiyo inatajwa kuongeza chachu ya Brendan Rodgers kutaka kufukuzwa kama atapoteza mchezo dhidi ya Everton.
Stori za kazi ya Brendan Rodgers kuwa mashakani kama atapoteza mchezo na wapinzani wake wa jadi Everton zilimfikia baada ya kuulizwa na waandishi vipi haogopi kufukuzwa kazi kama akipoteza mchezo dhidi ya Everton katika uwanja wa Goodison Park?
“Hapana
tutaingia uwanjani tukiwa na dhana moja tu ya kucheza vizuri na
kushinda, kama tutaingia na bahati nzuri tunaweza kushinda mchezo,
kuhusu suala la kufukuzwa siogopi kufukuzwa sio kwa sababu ni kiburi au
nimehakikishiwa kuwa siwezi kufukuzwa. Nitafanya kadri ya uwezo wangu
kuhakikisha tunashinda”>>> Brendan Rodgers

Note: Only a member of this blog may post a comment.