MWANADADA ‘kiraka’ anayefanya mitindo, muziki, uigizaji
na ujasiriamali, Jokate Mwegelo amemwaga chozi baada ya kupata taarifa
za kukosa ubunge wa Jimbo la Ukonga kwa aliyekuwa Meya wa Ilala, Jerry
Silaa na kusema ameumia kuliko maelezo.
Akizungumza na Ijumaa juzi, Jokate ambaye ni mtu wa karibu sana na
mheshimiwa huyo alisema, hakutarajia kabisa kupata matokeo hayo lakini
akadai anachoamini bado ‘mtu’ wake huyo ana nafasi ya kupata cheo
kingine.
“Mimi nina imani kuwa atapata nafasi nyingine nzuri kwani uwezo wa kuongoza anao lakini nimeumia sana, yaani dah!” alisema Jokate.
“Mimi nina imani kuwa atapata nafasi nyingine nzuri kwani uwezo wa kuongoza anao lakini nimeumia sana, yaani dah!” alisema Jokate.
Note: Only a member of this blog may post a comment.