Tukio limetokea Mwembechai, Dar es salaam ambapo awali inasemekana kuwa alipotea katika mazingira ya kutatanisha.
Mjomba wa marehemu amezungumza kwenye Hekaheka na kusema alifikiwa na taarifa akiwa kazini kwake Kariakoo..akaamua kutoka na kwenda eneo la tukio.
Anasema walipewa taarifa kuwa ndugu yao huyo alipotea na wakaamua kumtafuta bila mafanikio ndipo walipoamua kwenda katika hospitali mbalimbali na walipomkosa wakatoa taarifa kituo cha Polisi lakini mke wa marehemu alikua hataki waende kutoa taarifa kituo cha Polisi Magomeni.
Mke katoa maelezo Polisi na kusema kuwa kuna jamaa alimpigia mume wake wakafanye biashara..baada ya muda jamaa akarudi na kumtafuta marehemu lakini hakuweza kumpata, mke aliamua kwenda nyumbani kwa mama yake na alikuta sandals za mume wake nje, alipomuuliza mama yake akaambiwa ameondoka na rafiki zake.
Msikilize hapa Mjomba wa marehemu akizungumza na Geah Habib..
Note: Only a member of this blog may post a comment.