Tuesday, October 6, 2015

Anonymous

Hekaheka ya Jirani Kuwatishia Wenzake Kutaka Kuwachinja Imesikika Leo…

Kwenye zile stori za hekaheka leo Geah Habib aliitwa na wnaanchi wa Kivule Geah wakidai kuna jirani yao amekuwa akiwanyanyasa na kutaka kuwachinja.

Watu wengi wamekuwa wakilalamika, kwanza wamesema kuna kiwanja chake ambacho sasa kimekuwa msitu na kuna nyoka wengi ambao wanahatarisha maisha yao..wamemuomba afyeke lakini amekataa.

Pia kuna siku mke wake alipandisha mashetani na kumtaja mmoja wa majirani zake kuwa anamloga..wakamfuata nyumbani kwake akiwa na familia yake na mapanga wakitaka kumuua jirani yake ambaye wanadai anawaloga.

Iliwabidi wakimbilie kituo cha polisi Kivule lakini wanachoshangaa mtuhumiwa na familia yake hawajakamata kwa madai Serikali haiamini uchawi..lakini madai yao ni kuvunjiwa nyumba na vitu vyao kuharibiwa sana.

Majirani wamezungumzia manyanyaso wanayoipata kutoka kwa mzee huyo na kusema amekuwa akiwanyanyasa sana ikiwemo kuwatishia kuwachinja akishirikiana na watoto wake.

Wanasema imefikia hatua akikuta uchafu katika viwanja vyake pamoja na pori lake anawaambia majirani zake waende kuokota na endapo watatakadi ataenda kuokota mwenyewe na kupeleka ndani ya nyumba zao.

Wamesema wanaiomba Serikali iingilie kati kwani imefikia hatua hata hataki nguzo zipite karibu na viwanja vyake na huwatoza fedha kubwa ambayo hawawezi kumudu.

Watoto wake pia wamekuwa wakitumia mapanga na kuwatishia watu kuwauua, pia wamekuwa wakiwatukana na kukimbilia kuwashtaki kwa baba yao endapo watawadhuru…kuna jirani mpaka sasa yupo ndani baada ya kugombana na familia yake.
Tunaomba radhi kutokana na tatizo la sauti

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.