Tuesday, October 6, 2015

Anonymous

Hamis KIIZA Kaingia Katika Historia ya Kuwa Mchezaji wa Kwanza wa SIMBA SC Kutwaa Tuzo Hii (+Pichaz)

Mwishoni mwa mwezi September klabu ya Simba ilitangaza mfumo mpya kwa klabu za Tanzania lengo likiwa ni kuinua morali kwa wachezaji wake na kujenga hali za kujituma kwa kuanzisha tuzo ya mchezaji bora wa mwezi. Rais wa klabu hiyo Evans Aveva alitangaza pia mfumo utakaokuwa unatumika katika kumpata mchezaji bora wa mwezi wa klabu hiyo.
5
Uongozi wa klabu hiyo ulitangaza mpango huo lakini jukumu la nani atapewa nafasi ya kuwa mchezaji bora wa mwezi alipewa shabiki na mpenzi wa klabu hiyo, kwani ndio mtu pekee aliyekuwa na nafasi ya kuchagua mchezaji yupi anastahili kuwa mchezaji bora wa mwezi kwa kupiga kura kwa njia ya SMS.
7
Ikiwa tuzo hizo ni mara ya kwanza kufanyika kwa klabu ya Simba, mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Hamis Kiiza ameweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwa tuzo hiyo kwa kupata kura 250 kati ya kura 411. Hamis Kiiza amekabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi na kocha wa Simba Dylan Kerr sambamba na Tsh laki 5.
-via millardayo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.