Licha ya picha zake za awali kumuonesha Cristiano Ronaldo akiwa katika ndege kuelekea Ureno kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Ureno, Ronaldo hakuishia kuungana na timu pekee kwani alitumia muda wake akiwa Ureno kuzindua brand mpya ya viatu vyake.
Ronaldo
anaonekana kujikita zaidi katika biashara kama za mavazi perfume na
kadhalika kwa kutumia umaarufu wake, kwani inaweza ikawa rahisi zaidi
kufanikiwa, awali Ronaldo
alizindua nguo za ndani, mashati, perfume na sasa ni wakati wa kuzindua
viatu vyake, huenda ukawa unajiuliza model gani anayemtumia kuuza
bidhaa zake.
Staa huyo wa Real Madrid ya Hispania amesimama mwenyewe kama model wa bidhaa zake, kuanzia nguo za ndani, perfume, shati na hata sasa viatu. Cristiano Ronaldo anaingia katika list ya watu maarufu waliowahi kuanzisha na kuuza bidhaa zao kwa kutumia majina yao. Brand mama ya Ronaldo ni CR7
Note: Only a member of this blog may post a comment.